Zambia imeomba Tanzania kuiuzia nchi hiyo ya jirani gesi asilia kwa madhumuni ya kuzalisha umeme na kupanua wigo wa uzalishaji wa viwandani. Aidha, Tanzania na Zambia zimekubaliana kuifufua Reli ya TAZARA kati ya nchi hizo mbili kwa kukabiliana ipasavyo na changamoto na matatizo ambayo kwa muda sasa yamekuwa yanakwamisha utendaji bora wa reli hiyo iliyojengwa kwa nia ya kuiwezesha Zambia …