Matukio Ziara ya Rais Kikwete Nchini Finland

UHUSIANO baina ya Tanzania na Finland ni wa kudumu na utaimarishwa na kutafutiwa namna ya kuukuza zaidi ya hapa ulipo sasa. Rais Sauli Niinisto wa Finland amemueleza Rais Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 2 Juni, Ikulu, jijini Helsinki wakati wa Mazungumzo baina ya viongozi hao. “Uhusiano wetu ni wa muda mrefu, ni uhusiano ambao umedumu kwa miaka 50, tumekuwa na uhusiano …