FIFA Kumchagua Rais Mpya 2016

SHIRIKISHO la soka duniani Fifa litaandaa kongamano la dharura kuchagua rais mpya tarehe 26 mwezi Februari 2016. Hii ni licha ya rais aliyeko sasa Sepp Blatter kutangaza nia ya kuondoka mamlakani wiki moja tu baada ya kuchaguliwa upya kuwa rais wa shirikisho hilo tarehe 26 mwezi Mei. Tangazo hilo lilifuatia juma lenye matukio na madai ya ulaji rushwa na ufisadi …

Madudu Yazidi ‘Kuibuka’ Ufisadi FIFA

UCHUNGUZI wa BBC umegundua jinsi zilivyotumika kiasi cha dola milioni 10 zilizotumwa kutoka FIFA kwenda kwa akaunti za aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner. Pesa hizo zilipangiwa kutumiwa na shirika moja la Afrika Kusini katika nchi za Caribbean. Lakini nyaraka ambazo zilikaguliwa na BBC zinasema kuwa bwana Warner alitumia pesa hizo kwa mikopo yake ya kibinafsi na …

CECAFA, TFF Wazungumzia Uchaguzi wa CAF na FIFA

RAIS wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) akiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wamezungumzia uchaguzi wa CAF na FIFA.   Rais Tenga ameishukuru familia ya TFF kwa kumuunga mkono katika …

FIFA, TFF Kutoa Kozi ya Ukufunzi Desemba

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameandaa kozi ya ukufunzi wa utawala itakayofanyika Desemba mwaka huu. Kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu, ambapo sifa ya chini ya elimu kwa wanaotaka kushiriki ni kidato cha nne. …