WATAFITI katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani. Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa. Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa …
Hadhi ya Tanzania Yapanda Katika Benki ya Afrika
TANZANIA imepandishwa hadhi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na sasa inaweza kupata mikopo mikubwa zaidi na yenye hadhi kubwa zaidi kuliko huko nyuma. Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo katika Tanzania, Bi. Tonia Kandiero ametangaza hayo, Julai 23, 2014. Bi. Kandiero amesema kuwa miaka yote tokea Tanzania kuwa mwanachama wa AfDB, imekuwa inapata mikopo ya hadhi ya chini zaidi …
Mtandao wa Wanawake na Katiba Wawanoa Wajumbe Bunge Maalum
Na Joachim Mushi MTANDAO wa Wanawake na Katiba nchini Tanzania umewakutanisha baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba pamoja na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba kujadili namna ya kushinikiza masuala ya haki za wanawake kuingizwa katika rasimu ya pili ya Katiba Mpya. Semina hiyo iliyoshirikisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wanahabari imeanza leo katika …
JK Mgeni Rasmi Siku ya Mashujaa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa itakayofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki amesema kuwa maadalizi ya sherehe hizo yamekamilika …
Rais Mstaafu Mwinyi Awaasa Watanzania
Na Aron Msigwa – MAELEZO RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, amewataka Watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao. Kauli hiyo ameitoa jana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea …
Rais Kikwete Awang’ang’ania Wezi Vyama vya Ushirika
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Serikali yake haitalipa madeni ambayo baadhi ya Vyama vya Ushirika nchini vinadaiwa na mabenki mpaka wezi waliosababisha madeni hayo wamekamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa baadhi ya maofisa wa Serikali hujidhalilisha kwa kujifanya mawakala wa wanunuzi …