Tusikubali Kugeuzwa Mtaji na Wanasiasa – Mizengo Pinda

  WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amewaonya Watanzania kuwa makini na watu wanaotumia rushwa ili kupata nafasi za uongozi na hasa kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, 2015. Pinda ametoa onyo hilo, Julai 27, 2014 wakati akizungumza na mamia ya waumini na viongozi mbalimbali waliohudhuria ibada ya uzinduzi wa dayosisi mpya ya Ruvuma ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri …

KATIBA MPYA: Wassira, Lipumba, Lissu ‘Wanyukana’

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wassira akiwakilisha CCM, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, jana walitoana jasho katika mdahalo wa Katiba ulioandaliwa na East African Business and Media Institute. Mdahalo huo uliohudhuriwa na watazamaji wapatao 500, ulikuwa na mada inayosema: ‘Nani anakwamisha Upatikanaji wa Katiba Mpya.’ Kila upande …

Wanafunzi Waalimu Watakiwa Kuvaa Nadhifu

Na Anna Nkinda – Maelezo, Nachingwea WANAFUNZI wa kike wa vyuo vya ualimu nchini wametakiwa kuvaa mavazi nadhifu yanayoendana na maadili ya kazi yao ili wanafunzi na jamii inayowazunguka ijifunze kutoka kwao kwani wao ni kioo cha jamii. Mwito huo umetolewa hivi karibuni na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na baadhi ya wanafunzi wa kike wa chuo cha Ualimu Nachingwea mara baada ya …

Wajumbe Bunge Maalum Kupigania Usawa na Mgawanyo wa Rasilimali

Na Joachim Mushi WAJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wameahidi kupaza sauti kupigania masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia pamoja na kusimamia usawa kwa jamii yote juu ya mgawanyo wa rasilimali ardhi, elimu, uongozi na huduma za kijamii. Kauli hiyo imetolewa leo na baadhi ya …