Na Mwandishi Wetu, Dar KWA watumishi wa umma uanzishwaji wa Watumishi Housing Company (WHC) ambao ni mpango wa makazi kwa watumishi wa umma ni mkombozi wa kweli kwa ustawi wa maisha ya mfanyakazi wa serikali, asante kwa serikali ya awamu ya nne kwa kuanzisha taasisi hii muhimu kwa ujenzi wa taifa. WHC ni taasisi inayojihusisha na uendelezaji miliki na usimamizi …
Watoto Wadaiwa Kumnyonga Mwenzao na Mumning’iniza Mtini
WAKAZI wa Kijiji cha Masusu, Kata ya Gisambalang wilayani Hanang’ katika Mkoa wa Manyara wamepatwa na mshtuko kutokana na tukio lenye utata la kuuawa mtoto Omary Hamis mwenye umri wa mitatu, kisha mwili wake kutundikwa juu ya mti. Inadaiwa kuwa Omary aliuawa na watoto wenzake wawili ambao ni wakazi wa kijiji hicho kwa kumpiga kwa fimbo kisha kumnyonga na baadaye …
Kikwete Nyota wa Demokrasia Afrika 2014, Apewa Tuzo
Na Mwandishi Maalum RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kwa mara nyingine ametunukiwa tuzo la kimataifa – zamu hii kwa kuwa mshindi wa Tuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika 2014 – Icon of Democracy Award Winner for 2014 in Africa. Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa Rais Kikwete na kupokelewa Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete amekuwa …
Ajali ya Basi la Morobest na Rori Yaua 17 na Kujerui 56
WATU 17 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Morobest namba za usajili T258 AHV lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam na Lori namba T820CKU na tela lake namba T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma inaeleza ajali hiyo imetokea …
Mabosi IMTU Mapanda Kizimbani, DPP Awafutia Mashtaka
SAKATA la kutupwa kwa viungo vya binadamu bila kufuata utaratibu jana liligeuka sinema wakati maofisa wanne wa Chuo Kikuu cha Tiba na Teknolojia (IMTU), walipofikishwa mahakamani Dar es Salaam. Maofisa hao ambao ni maprofesa na wahadhiri wa chuo hicho walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kufukia viroba 83 vya miili ya binadamu. …
Matumizi ya Tiketi Mtandao; SUMATRA Waiumbua CHAKUA
Rose Masaka – MAELEZO Dar es Salaam MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imepinga kwamba haiwezi kuwalazimisha abiria wa mikoani kutumia mchakato wa mbinu mpya ya ukatishaji wa tiketi za mabasi ya kwenda mikoani kwa njia ya mtandao ikiwemo ya simu za mkononi kwa kuwa baadhi ya wamiliki wa mabasi wamegawanyika juu ya mfumo huo licha ya kuwa haukidhi mahitaji …