Serikali Yaivunja Rasmi Tume ya Jaji Jeseph Warioba

RAIS aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katika kwa mujibu wa kifungu cha 5 na 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 kwa Tangazo la Serikali Na.110 la Mwaka 2012. Tume ilikusanya maoni na kuandaa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo imewasilishwa kwenye Bunge Maalum. Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya …

Rais Kikwete Awataka Viongozi Tanga Kusimamia Watoto Shule

RAIS Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule, wana kwenda shule bila kukosa hata kama hawana uwezo wa kumudu mahitaji maalum ya shule. Rais amesema hayo Wilayani Korogwe wakati akipokea taarifa ya Wilaya iliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Bw. Mrisho Gambo. Katika taarifa yake kwa Rais, Bw. Gambo ameelezea hali ya mdondoko …

Maisha ya ‘Geto’ Changamoto kwa Wanafunzi Sekondari za Kata Tanga

UJENZI wa Sekondari za Kata katika mikoa mbalimbali umesogeza huduma za elimu kwa baadhi ya maeneo. Ipo mikoa ambayo awali ilikuwa na shule chache za sekondari hali ambayo ilifanya wanafunzi wachache kupata fursa ya kujiunga na sekondari. Kwa sasa hali si hivyo tena, mikoa mingi imeongeza idadi ya shule hizo licha ya changamoto kibao inazozikabili shule hizi. Zipo baadhi ya …

Hotuba ya Rais Kikwete Yaliweka Bunge la Katiba Njiapanda

KWA neno moja unaweza kusema kwamba wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na wananchi kwa ujumla wako “njiapanda”. Hii ni baada ya hotuba ya ufunguzi wa Bunge hilo iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuibua mambo mazito ambayo kimsingi yanatofautiana na mapendekezo yaliyomo katika Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa bungeni na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. Huku …

Mawakala Redio za Jamii Wataja Mafanikio Mradi wa SIDA

Na Mwandishi Wetu, Pangani MAWAKALA wa redio za jamii wanaoshiriki mafunzo mbalimbali yanayofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wametaja mafanikio waliyoyapata kutokana na mradi unaotoa uwezo wa matumizi wa tehema katika redio jamii katika upashaji wa habari. Wakitoa tathmini ya maendeleo ya mradi katika …

Wabunge Bunge la Katiba Wasema JK Hajavuruga Mchakato wa Katiba

Na Magreth Kinabo – Maelezo, Dodoma   UMOJA wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba la Tanzania Kwanza umesema kuwa hotuba ya Rais, Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa Bunge Maalum la Katiba hivi karibuni, haikuingilia wala kuvuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya, bali kiongozi huyo alitoa maoni na ushauri kama kiongozi wa nchi. Aidha wajumbe hao wamesema Rais Kikwete hakuingilia kanuni za bunge …