Anne Makinda Awataka Wanawake Kujenga Hoja na Kuzitetea

Na Magreth Kinabo –MAELEZO, Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Anne Makinda ametoa changamoto kwa wajumbe wenzake wanawake walio kwenye Bunge hilo,  kujenga hoja zenye nguvu zinazohusu masuala yanayohusu wanawake na kuzitetea  kwa sauti moja ili ziweze kupita katika Rasimu ya Katiba. Kauli hiyo imetolewa na Anne ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  …

Mama Tunu  Pinda awaasa wanandoa

MKE WA WAZIRI MKUU Mama Tunu Pinda amewaeleza wanandoa kuwa ndoa ndiyo taasisi ya kwanza kuwafundisha watu maadili na kumjua Mungu pasipo Mungu haiwezekani. Amesema hayo wakati akifungua rasmi semina ya wanandoa wa kuanzia siku moja hadi miaka 25 iliyoandaliwa na watoa huduma wa New Life in Christ (Maisha Mapya Ndani ya Kristo) jana mchana tarehe 29 Machi, 2014 katika …

Dk Maria Kamm Aibuka Mwanamke bora wa Mwaka

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wanawake walioteuliwa kwenye Tuzo ya Mwanamke Bora wa mwaka 2013/2014 wasibweteke bali waendeleze juhudi zao na wazidi kung’ara zaidi.   Ametoa wito huo jana usiku (Jumamosi, Machi 29, 2014) kwenye hafla ya kumtuza mwanamke bora wa mwaka 2013/2014 iliyofanyika kwenye ukumbi wa African Dream nje kidogo ya mji Dodoma.   “Lazima muendelee kuonekana mnazidi …

“Kifo Hakizoeleki” Wassira

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano), Bw. Stephen Wassira aliwavunja mbavu waombolezaji waliofika kwenye mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara marehemu John Gabriel Tuppa yaliyofanyika nyumbani kwake Kilosa mjini, mkoani Morogoro. Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Mara, Bw. Wassira alisema watu wote waliohudhuria mazishi hayo wanataka kwenda peponi lakini tatizo ni …

TGNP Mtandao Wafunga Warsha ya Siku 3 kwa Waandishi wa Habari Shinyanga

Kaimu meneja wa habari na mawasiliano kutoka TGNP Mtandao bi Kenny Ngomuo  akizungumza leo katika ukumbi wa papa Paulo wa pili Ngokolo mjini Shinyanga wakati katika siku ya mwisho ya warsha ya siku tatu kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ambayo imeanza tarehe 27,2014 ikiwa na lengo la kupanua uelewa kuhusu harakati za ukombozi wa wanawake katika muktadha wa …