Na Magreth Kinabo- Dodoma MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ametangaza rasmi majina mengine ya ziada ya wajumbe wapya wa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo. Majina hayo yametangazwa leo na Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Hassan Suluhu mjini Dodoma kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bunge hilo. Taarifa hiyo ilieleza kwamba Sitta amefanya uteuzi huo, …
BRN Yaendeleza Mapinduzi ya Kilimo
Na Hassan Abbas MPANGO wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaosimamiwa na Kitengo cha Rais cha Utekelezaji wa Miradi Mikubwa (PDB), umeendelea kupata mafanikio katika kuhakikisha mapinduzi ya kilimo nchini. Akitoa mada jana (Alhamisi) Dar es Salaam katika mkutano wa siku tatu unaohusisha wadau wa sekta ya kilimo kutoka nchi mbalimbali, Naibu Mtendaji Mkuu wa PDB, Bw. Peniel Lyimo alisema tayari …
Baadhi ya Wajumbe Bunge la Katiba Wataka Serikali Mbili
Na Magreth Kinabo – Maelezo Dodoma BAADHI ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wamependekeza kuwepo kwa Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye mfumo wa Serikali mbili, wakati wa kuchambua sura ya kwanza na ya sita zilizoko katika Rasimu ya Katiba mpya. Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na wenyeviti wa Kamati namba 10 na namba moja ya Bunge hilo wakati …
TFDA Yatoa Tahadhari kwa Watumiaji Bidhaa za Madukani
Na Aron Msigwa – MAELEZO MAMLAKA ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) imewataka wananchi kujenga utaratibu wa kusoma maelezo ya bidhaa za vyakula zinazouzwa madukani ili kubaini nchi zilikotengenezwa bidhaa husika, muda wa matumizi na taarifa za uthibitisho wa bidhaa hizo kutoka mamlaka hiyo ili kuepuka madhara yatokanayo na matumizi ya bidhaa zisizokidhi viwango. Hatua hiyo imekuja kufuatia ukaguzi wa maduka …
Machangudoa: Wabunge wa Katiba Wanatulipa Vizuri Kuliko Wateja Wengine
WASICHANA wanaofanya biashara ya kujiuza katika maeneo mbalimbali mjini hapa (Dodoma) wameelezea neema iliyowafikia kufuatia kujikusanyia pesa ndefu kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba ambao wanadaiwa kuwalipa vizuri. Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, wadada hao ambao baadhi wanatokea Mikoa ya Dar, Arusha, Mbeya na kwingineko walisema kipindi hiki wanakiita ni cha mavuno kwao kwani waheshimiwa hao …
ADMISSIONS TO BASIC CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSES IN GENDER AND DEVELOPMENT AND BRIDGING COURSES AT GTI, 2014
ADMISSIONS TO BASIC CERTIFICATE AND DIPLOMA COURSES IN GENDER AND DEVELOPMENT AND BRIDGING COURSES AT GTI, 2014 GTI Centre for Feminist Leadership (GTI CFL) is a gender training institute registered under NACTE to offer courses under National Technical Awards since 2008. It is a subsidiary organization of TGNP Mtandao. GTI offers a diploma course in Gender and Development administered in …