Tanzania Kuadhimisha Wiki ya Elimu

Na Mwandishi Wetu KATIKA kutekeleza Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya Elimu, Serikali itawazawadia wanafunzi na shule zilizofanya vyema katika mitihani ya Elimu ya msingi na Sekondari. Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam Jumatatu April 14, 2014 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Dk. Shukuru Kawambwa alipozungumzia na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya …

Ikulu Yatoa Pole Kifo cha Muhidini Gurumo

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha mwanamuziki maarufu na wa siku nyingi, Muhidini Maalim Gurumo kilichotokea tarehe 14 Aprili, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa moyo uliomsumbua kwa muda …

Mafuriko Dar Yaua Watu Nane, Polisi Watumia Mbwa Kusaka Miili Zaidi…!

Na Joachim Mushi, Dar es Salaam MVUA Kubwa inayoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam ambayo imesababisha mafuriko imeua zaidi ya watu nane maeneo mbalimbali yaliyokubwa na mafuriko hayo. Kwa mujibu wa taarifa ambazo dev.kisakuzi.com imezipata kutoka kwa baadhi ya vikosi vya uokoaji watu nane wamebainika kufariki dunia huku kukiwa na tetesi ya idadi hiyo kuongezeka kutokana na taarifa zinazoendelea kukusanywa. …

Wizara ya Afya Yaandaa Mpango wa Matibabu kwa Watanzania Wote

Na Magreth Kinabo, Dodoma   SERIKALI iko katika mchakato kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Ugharamiaji Huduma za Afya kwa wananchi ili kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma za afya za msingi bila vipingamizi vyovyote vya kifedha. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid wakati wa ufunguzi wa kukusanya maoni ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu …

Mradi wa SECO Wazinduliwa Mkoani Arusha

MRADI wa kuunganisha sekta za Wazalishaji matunda, mbogamboga na wenye hoteli (SECO)unaofadhiliwa na Serikali ya Switzerland umezinduliwa Jijini Arusha. Mradi huo ambao lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya Watanzania wanaojihusisha na sekta hizo kwa kuongeza uzalishaji wao na uhakika wa masoko ya ndani na nje yanchi, unaanza utekelezaji wake mara moja ukiwa na thamani ya jumla ya Dola za …