Waziri wa Fedha Awataka Wafanyakazi Wizara Yake Kujituma

Na Eleuteri Mangi – MAELEZO WAFANYAKAZI wa Wizara ya Fedha wametakiwa kufanyakazi kwa bidii na kujituma kwa moyo wote ili kukuza uchumi wa nchi na taifa na hatimaye liweze kusonga mbele na kufikia malengo yake. Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum alipokuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kufungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa wizara …

Rais Kikwete Awataka Ukawa Warudi Bungeni, Awataka Wajumbe Kuacha Matusi

Na Joachim Mushi RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewataka wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda kundi la UKAWA waliogoma kuendelea na majadiliano ya kuandaa katiba mpya katika bunge la katiba kurudi bungeni na kuendelea na majadiliano. Rais Kikwete ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika viwanja vya sabasaba alipokuwa akilihutubia taifa kwa kuzungumza na vijana na kupokea maandamano …

Mahafali ya Pili Chuo cha Mafunzo ya Jinsia Tanzania Yafanyika

Na dev.kisakuzi.com, Dar es Salaam MAHAFALI ya pili ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) yamefanyika leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo hicho eneo la Mabibo. Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 9 wamehitimu mafunzo ya njinsia ngazi ya cheti. Akizungumza kabla ya kuwatunuku vyeti, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Jinsia, Asseny …

Wanavijiji Mbeya Walaumiana Udhibiti wa Mimba kwa Wanafunzi

Na Joachim Mushi, Mbeya Vijijini WANAVIJIJI wa vijiji vya Shibolya, Usoha Njiapanda, Simambwe, Ikhoho na Ilembo Usafwa vyote vya wilayani Mbeya Vijijini wametupiana lawama kuhusiana na baadhi ya wazazi na viongozi wa vijiji kuwa wakifumbia macho watu wanaotuhumiwa kuwatia mimba wanafunzi wa msingi na sekondari na kuwakatisha masomo. Kauli hiyo imetolewa juzi na baadhi ya wanakijiji walipokuwa wakifanya mazungumzo na …