Na Magreth Kinabo, Maelezo MSEMAJI wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene amesema Jaji Joseph Warioba alitunukiwa tuzo ya muungano iliyotukuka kwa kuwa alistahili, kama viongozi wengine na si kweli kwamba kitendo hicho ilikuwa kumkejeli kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti hivi karibuni. Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Mwambene wakati akizungumza na waandishi …
Mzee Auwawa Kikatili Wilayani Rombo
MKAZI wa Kijiji cha Mahida Nguduni, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Dominick Kavishe (65) mkulima ameuwa kikatili kwa kuchomwa na vitu vyenye ncha kali katika sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wasiofahamika. Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu na mtandao huu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa kwa …
Vifo vya Watu 19 katika Ajali Singida Vyamgusa Rais Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Singida, Perseko Kone kufuatia vifo vya watu 19 wakiwemo Askari Polisi wanne (4) na Viongozi watatu wa Kijiji kufuatia ajali ya barabarani iliyosababishwa na basi lililokuwa likitokea Kigoma kuelekea Dar es Salaam katika Barabara kuu ya Singida – Dodoma. Ajali hiyo ilitokea …
Basi Laua Trafiki Wanne, Viongozi wa Kijiji, Ndugu 10, 55 Wanusurika Kifo
WATU 19 wakiwamo askari polisi wanne wa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani Singida wamekufa papo hapo baada ya kugogwa na basi la Sumry lililokuwa linatoka Kigoma kwenda Dar es Salaam. Wengi waliofariki katika ajali hiyo, iliyotokea juzi saa tatu na nusu katika Kijiji cha Utaho, Tarafa ya Ihanja mkoani Singida, ni wa ukoo mmoja wa Bulali. Watu hao pamoja na …
Bilioni 111 Zatumika Kununua Mazao kwa Wakulima.
SERIKALI imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 111 kununua mazao kwa wakulima katika kipindi cha mwaka 2013/2014 ikiwa ni malipo kwa wakulima baada ya kuiuzia nafaka Serikali. Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akieleza mafanikio yaliyofikiwa …
CHADEMA, CUF, na NCCR-Mageuzi Kushirikiana Uchaguzi 2015
*Kusimamisha mgombea mmoja wa urais 2015 VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeanza maandalizi ya kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, gazeti hili limebaini. Kadhalika, vyama hivyo ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi na CUF vinakusudia kuwa na mgombea mmoja wa nafasi za wabunge na madiwani, ikiwa ni hatua ya kuzikabili …