AZAM FC Wampelekea Rais Kikwete Kombe…!

Na dev.kisakuzi.com, Dar es Salaam TIMU ya Mpira wa Miguu ya Azam FC ambao ni mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara, jana jijini Dar es Salaam ilimpelekea kombe la Ubingwa huo Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Azam inayomilikiwa na kampuni maarufu na tajiri Afrika Mashariki ya mfanyabiashara, Said Salim Bakhresa (SSB) inayotengeneza bidhaa mbalimbali nchini …

Wafanyakazi 32 Waibuka Wafanyakazi Bora, Wakabidhiwa Fedha..!

Na Joachim Mushi JUMLA ya wafanyakazi 32 kutoka makampuni, taasisi na idara mbalimbali nchi  wamepewa dhawadi ya vyeti pamoja na fedha viwango tofauti baada ya kuibuka wafanyakazi bora na hodari kitaifa katika kampuni na taasisi wanazofanyia kazi. Majina ya wafanyakazi hao yalitajwa jana jijini Dar es Salaam pamoja na kukabidhiwa zawadi zao kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, zilizofanyika …

Wananchi waomba Kituo cha Afya Simambwe Kufanya Kazi Saa 24

Na Joachim Mushi, Tembela, Mbeya WANANCHI wa Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini wameiomba Serikali kusaidia kukiwezesha Kituo cha Afya Simambwe ili kifanye kazi saa 24 ili kuwasaidia muda wote wananchi wanaohudumiwa na kituo hicho hasa wajawazito. Kauli za ombi hilo zimetolewa hivi karibuni kwa nyakati tofauti na wananchi hao walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa habari hizi katika vijiji …

Wafanyakazi Walia na Kodi Mei Mosi, Serikali Yaahidi Kupandisha Mishahara…!

Mmoja wa viongozi kutoka chama cha waajili Tanzania. Na Joachim Mushi, Dar es Salaam WAKATI Serikali ikiahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) limeitaka Serikali kuonesha dhamira ya kweli ya kupunguza viwango vya kodi kwa wafanyakazi kwani hali hiyo inazidisha makali ya maisha kwa wafanyakazi. Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la …

Sherehe za Mei Mosi Zaingia Dosari, Mfanyakazi wa Ikulu ‘Afia’ Uwanjani…!

Na Mwandishi Wetu MAADHIMISHO ya Siku ya Wafanyakazi Kitaifa, maarufu kama Mei Mosi yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam yameingia dosari baada ya mmoja wa wafanyakazi kufariki dunia uwanjani kwa ghafla akiwa katika maadhimisho hayo. Mfanyakazi huyo anayedaiwa kufanyakazi Ikulu alizidiwa ghafla akiwa katika maandamano na kupatiwa huduma za kwanza lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na hatimaye kudaiwa kupoteza …