MTU mmoja amejeruhiwa baada ya kulipukiwa na kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Ziwa Victoria, Makongoro Misheni, Mwanza. Aliyejeruhiwa ni mhudumu wa nyumba ya wageni ya kanisa hilo, Benadeta Alfred (25) aliyekumbwa na mkasa huo juzi saa mbili usiku. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alisema jana …
Mahabusu Wavua Nguo Mhakamani Kupinga Wenzao Kuachiwa
MAHABUSU wa Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha, jana walizua tafrani katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini hapa, baada ya kuvua nguo na kugoma kushuka kwenye basi wakipinga kitendo cha watuhumiwa wawili wa dawa za kulevya kuachiwa kinyemela. Watuhumiwa wanaolalamikiwa ambao mashtaka yao yalibadilishwa mara mbili ili wapewe dhamana ni Dharam Patel (26) na Nivan Patel (20) wanaodaiwa …
JK Aenda Abuja Kwenye Mkutano wa Uchumi
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka leo tarehe 6 Mei, 2014 kuelekea Abuja, Nigeria kuhudhuria Mkutano wa siku 3 wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika (World Economic Forum). Mkutano huo unaoanza kesho tarehe 7 – 9 Mei, 14, utahudhuriwa na viongozi kutoka Afrika na duniani kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine mkutano utajadili njia mbalimbali zitakazolifanya Bara la Afrika kuumudu ukuaji wa …
Serikali Kuja na Mpango wa Kutibu Magonjwa Yasiopewa Kipaumbele
Na Magreth Kinabo – Maelezo SERIKALI inaandaa mpango wa kutoa huduma za magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTD,s) kwa pamoja ili kuweza kufikia watu wengi kwa kupunguza gharama. Hayo yamasemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Neema Rusibamayila wakati akifungua mkutano wa tatu wa wa siku tatu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo unaoendelea kwenye hoteli …
Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014
Na Mwandishi Wetu Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema lengo la mchakato wa Katiba ni kuhakikisha kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo ni bora zaidi kuliko zote itakayoshughulikia changamoto na kuweka mazingira ambayo yatamrahisishia maendeleo mwananchi kwa haraka. Akitoa risala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha, …
Mabasi ya Kasi Dar Kuanza Mwishoni mwa 2014
Na Frank Mvungi- Maelezo SERIKALI inatarajia kuanza kutoa huduma za awali (interim services) katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART) kutoka Kimara mwisho hadi Kivukoni jijini Dar es Salaam mwaka 2015 baada ya miundombinu kukamilika. Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Wakala wa mabasi yaendayo Haraka (DART), William Gatambi wakati wa mkutano na waandishi wa habari jana jijini Dar es …