*Ni kile kinachomilikiwa na mwekezaji anayejenga kiwanda Mtwara RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametumia siku ya Mei 9, 2014, kutembelea kiwanda kikubwa zaidi cha saruji kuliko kingine chochote duniani cha Dangote Cement Obajana Plant na kinachomilikiwa na tajiri mkubwa zaidi wa Afrika, Aliko Dangote, ambaye pia anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mjini Mtwara. Akiandamana na …
TGNP Mtandao ya Chambua Bajeti na Wahariri wa Vyombo vya Habari
Juu ni baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa na wataalamu wa masuala ya uchambuzi wa bajeti kwa mrengo wa kijinsia. Mada ikiwasilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa TGNP Mtandao
Serikali Haijawatimua Kazini Maprofesa Kideghesho na Songorwa
SERIKALI inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa potofu zinazoendelea kuchapishwa na kutangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Watumishi Waandamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Alexander Songorwa ambaye ni Mkurugenzi, Idara ya Wanyamapori na Prof. Jafari Kideghesho, Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori. Kumekuwa na taarifa kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba Wakurugenzi hao walikuwa …
Mipango ya Wanajamii ni Muhimu Katika Kusimamia Wanyamapori – UNDP
KIONGOZI wa UNDP aliyeko ziarani nchini Tanzania, Helen Clark, amesema usimamizi wa maliasili unaoshirikisha jamii ni ufumbuzi wa muda mrefu na wenye ufanisi zaidi kwa ujangili wa tembo na biashara haramu ya wanyamapori. Akizungumza na watu kutoka vijiji 21 karibu na Hifadhi ya Taifa Ruaha alijifunza uzoefu wao na changamoto za usimamizi katika uhifadhi wa wanyamapori. ‘Ni wazi,’ alisema, ‘kila …
Walimu Wapya Wilaya ya Handeni Waonja Joto ya Jiwe
Na Joachim Mushi WAAJIRIWA wapya wa fani ya ualimu wa shule za msingi katika Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga wameanza kazi kwa kuonja machungu ya madeni baada ya kutopewa stahili zao zote kabla ya kuanza kazi na kusambazwa kwenye vituo vyao vya kazi kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. Wakizungumza na dev.kisakuzi.com kwa masharti ya kutotaja majina yao kwa …
Rais Kikwete Awasilisha Rambirambi za Watanzania kwa rais wa Nigeria
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Mei 8, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan katika Hoteli ya Transcorp Hilton katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Abuja. Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete kwa mara nyingine, amewasilisha rambirambi rasmi za Tanzania, za Watanzania na za kwake mwenyewe kwa kiongozi huyo wa Nigeria kufuatia …