Mkuu wa Mkoa, Meya Dar Wafanya Usafi Mto wa Mlalakuwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na wananchi kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa …

Jamii Forums Wawavuta Wengi Maonesho ya Biashara ya Uturuki

KAMPUNI ya Jamii Media wamiliki wa mitandao maarufu ya mijadala kwa jamii kupitia mitandao ya jamii, JamiiForums na Fikra Pevu nchini Tanzania imevuta watazamaji wengi kutembelea banda lao lililoshiriki katika Maonesho ya Biashara ya Bidhaa za Uturuki na Tanzania yaliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee. Wananchi wengi waliotembelea katika maonesho hayo walikuwa wakipita katika banda la …

Dawa za Kinga ya Ukimwi Zatumiwa Vibaya na Machangudoa

WANAWAKE wanaofanya biashara ya kuuza miili na wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja sasa wanatumia dawa za kufubaza makali ya Virusi vya Ukimwi aina ya Truvada kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo badala ya kutumia mipira ya kondomu. Mwananchi lilizungumza na baadhi ya wafanyabiashara ya ngono jijini katika maeneo ya Mwananyamala Hospitali, Komakoma na Vingunguti ambao walisema kuwa …

Askari wa JWTZ Brian Salvatory Rweyemamu Kuzikwa Leo Dar

ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Private Brian Salva Rweyemamu aliyefariki dunia Mei 15, 2014 katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu anatarajiwa kuzikwa leo. Marehemu Private Brian Rweyemamu ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu atazikwa katika makaburi ya Kinondoni ya Jijini Dar es Salaam mchana. …

Ajali ya Malori Yafunga Barabara ya Mandela…!

Ajali ya malori ya mizigo imefunga barabara ya Mandela kwa muda. Ajali hiyo ilitokea jana jijini Dar es Salaam karibu na eneo la Tabata Dampo. Kwa mujibu wa mashuhuda walisema lori lililoburuzwa lilikuwa likivuka barabara ya mandeka kutokea viwandani na lingine likitokea Buguruni kuelekea Ubungo kwenye barabara ya Mandela. Dereva mmoja alijeruhiwa kidogo na kwenda kutibiwa. Ajali hii ilifunga barabara …

Werema Alikoroga, Alinywa: Atoa Kauli ya Kuwabagua Wazanzibari

KWA maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema ‘amelikoroga na kulinywa mwenyewe’, baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka. Kauli iliyoonyesha kuwagawa wabunge katika mafungu mawili; wa bara na Zanzibar, ilimlazimu Jaji Werema baadaye kusimama bungeni …