Serikali Kujenga Miundombinu Mipya ya Maji

Na Aron Msigwa – MAELEZO SERIKALI itaendelea na zoezi la kujenga miundominu mipya ya maji na kukarabati ile iliyopo ili kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi na salama katika maeneo mbalimbali nchini inawafikia wananchi wengi zaidi. Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Injinia Mbogo Mfutakamba wakati wa akizindua chapisho la …

Japan Yaahidi Kuendelea Kuchangia Bajeti ya Tanzania

Mwandishi Maalum, Tokyo SERIKALI ya Japan imeelezea nia yake ya kuendelea kuchangia bajeti ya Tanzania na kufafanua kuwa, inafanya hivyo kwa kutambua kuwa Tanzania ni mshirika mkubwa wa maendeleo na kwamba ni nchi yenye kutia matumaini katika kupiga hatua za kimaendeleo. Akizungumza jana katika Ofisi yake jijini Tokyo, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Japan Mheshimiwa Yoshihide Suga alisema, serikali …

UDA Kutumiwa na Wanafunzi kwa Vitambulisho Maalum

Na Anna Nkinda – Maelezo WILAYA ya Kinondoni kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaandaa mkakati wa kusafirisha wanafunzi kwa vitambulisho maalum vya wanafunzi kwa bei naafuu kwa kutumia mabasi ya UDA  kwenda shule za pembezoni. Hayo yamesemwa hivi karibuni na Ofisa Elimu Sekondari wilaya ya Kinondoni Omath Sanga wakati akisoma taarifa ya Idara …

Vifo vya bomu Nigeria vyafikia 118

Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos. Mabomu mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imefichwa ndani ya gari na kulipuka katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali. Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo. Kufikia sasa hakuna …

Wabunge Wataka Kikwete Aunde Tume ya Elimu

BAADHI ya wabunge jana walichachamaa wakisema elimu nchini ipo mahututi na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya kudumu ya elimu itakayochunguza mfumo wa elimu nchini. Wabunge hao walikuwa wakichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 iliyowasilishwa na waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa Jumamosi usiku. Mbunge …