Na Eleuteri Mangi – MAELEZO SERIKALI imetenga fungu la fedha ambalo litagawiwa kwenye vituo vyote vinavyotoa ushauri nasaha na kurekebisha watoto walio chini ya umri wa miaka 18 (mahabusu) zilizopo chini ya Idara ya Ustawi wa jamii nchini. Kauli hiyo imetolewa na Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja kufuatia habari iliyochapishwa na gazeti la Majira …
UKAWA Wamtaka Rais Kikwete Kusitisha Bunge la Katiba
UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umemtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha Bunge Maalumu la Katiba linaloendelea mjini Dodoma na iwapo hatafanya hivyo utaongoza maandamano nchi nzima. Umoja huo pia umeeleza kuwa kuendelea kwa Bunge hilo ni sawa na kuvuruga mchakato wa kupata Katiba Mpya, kuiweka nchi rehani, kufuja fedha za walipakodi, kuwahadaa Watanzania kwa kupitisha Katiba isiyotokana na maoni yao, …
Manispaa Kinondoni Yaitaji Bil. 1.3 Ujenzi wa Maabara
MANISPAA ya Kinondoni inahitaji jumla ya Shilingi bilioni 1.3 ili kutekeleza agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyezitaka halmashauri zote kuhakikisha zinajenga maabara katika shule za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu. Hayo yamebainishwa jana Jijini Dar es salaam na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Songoro Mnyonge wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja …
Mbunge UKAWA Asema Hofu ya Mungu Imemrudisha Bungeni
Na Magreth Kinabo, Dodoma MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba, Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amezitaja sababu za kurejea katika bunge hilo, kuwa ni hofu ya Mwenyezi Mungu. Aidha Arfi ameitaja sababu nyingine ni kwamba amerudi katika Bunge hilo, ili kuhakikisha kwamba anaisadia nchi kupita katika mchakato wa …
Rais Kikwete Aeleza Siri ya Utulivu na Amani Tanzania
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Tanzania imeendelea kuwa nchi tulivu, yenye umoja na amani kwa sababu ya sera nzuri ambazo zilianzishwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na ambazo zimeendelezwa na viongozi wakuu ambao walimfuatia Mwalimu. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania imefanikiwa kudumisha umoja, mshikamano na utulivu kwa sababu ya kuwa na …
Mtoto Amuua Baba Yake kwa Rungu
MTU mmoja mmwenye umri kati ya 65-70 ameuawa baada ya kupigwa na Rungu kichwani na mtu anayedaiwa kuwa ni mtoto wake, Mkazi wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro. Ofisa Mtendaji wa Kijiji Cha Ikuini, Gaspar Kauki amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba limetokea mnamo Agosti 8, mwaka huu majira ya saa nne usiku katika kitongoji cha Imongoni Kijiji cha …