TGNP Mtandao wamekutana na Kamati za Bunge Mjini Dodoma katika warsha ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo. Warsha hiyo ililenga kuwawezesha Wabunge zaidi ya 100 kushiriki katika kuhakikisha bajeti inayoandaliwa na Serikali inakuwa katika mrengo wa kijinsia. Semina hiyo pia imelenga kuwawezesha wabunge kutambua masuala yanayowakabili wanawake na makundi yaliyoko pembezoni na kudai yaingizwe kwenye bajeti ikiwemo …
Baba Amuua Mwanaye kwa Adhabu Kali
*Ampaka pilipili machoni na makalioni SIMANZI, vilio na majonzi vilitawala Kijiji cha Misiri, Kata ya Bugarama, wilayani Geita, kutokana na tukio la kifo cha mtoto, John Wiliam (4) aliyefariki baada ya kupewa adhabu na baba yake mzazi. Ilidaiwa kwamba mtoto huyo alifariki baada ya kuchapwa fimbo mwili mzima, kupigwa ngumi na mateke, kisha kupewa adhabu ya kukimbia riadha kuzunguka nyumba …
Lissu Awataja Mawaziri, Wabunge Walioomba Fedha LAPF
MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amewataja kwa majina mawaziri na wabunge aliosema bungeni kuwa wamekuwa ombaomba katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Baadhi ya waliotajwa ni pamoja na Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu wa Bunge), William Lukuvi; Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, …
Mzindakaya Agoma Kumsamehe Mbunge wa CCM Mkutanoni, Pinda Atoa Kauli Nzito…!
MBUNGE wa zamani wa Jimbo la Kwela, Chrisant Mzindakaya amekataa kumsamehe hadharani Mbunge wa sasa wa Sumbawanga Mjini, Bw. Aeshi Hilali baada ya kupewa fursa ya kushikana mikono jukwaani na kusameheana. Mzindakaya alikataa kufanya hivyo akisema yeye ni mkristu lakini hakuwa ameandaliwa kiroho kwa ajili ya tukio hilo. “Hapa ni shughuli ya kanisa na si mkutano wa Chama. Lazima …
Pinda Awataka Viongozi Rukwa Kumaliza Tatizo la Madawati
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameutaka uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha unamaliza tatizo la upungufu wa madawati ili watoto wa shule za msingi wasiendelee kukaa chini. Ametoa agizo hilo Mei 24, 2014 wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Rukwa mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa huo, Ikulu ndogo, mjini Sumbawanga. Waziri Mkuu amewasili mkoani Rukwa jana …
Madiwani Wawabana Watendaji wa Vijiji na Kata Rombo
BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo limetoa utaratibu mpya wa kuwabana watendaji wa vijiji na kata wasio toa taarifa za mapato na matumizi kwa wanakijiji wao ambapo kwa sasa watakuwa wakiwasilisha taarifa hizo katika kikao cha awali cha baraza la madiwani. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, Protasi Lyakurwa ambaye pia ni …