Utumbo wa Pacha Aliyekuwa Ameungana na Mwenzake Uko Nje

MMOJA wa watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana na kutenganishwa kwa upasuaji nchini India, hali yake ni mbaya na utumbo wake mkubwa sasa umetoka nje. Mtoto huyo Eliud Mwakyusa na mwenzake Elikana walizaliwa Februari 20, 2013, Kyela, Mbeya wakiwa wameungana kiunoni na Serikali iliwapeleka India ambako walitenganishwa. Walirejea Februari, mwaka huu na kusherehekea siku yao ya kuzaliwa wakiwa Hospitali ya Taifa …

Mama Mzazi wa Zitto Kabwe Afariki Dunia, Asafirishwa…!

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (CHAWATA), Shida Salum, ambaye pia ni mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, amefariki dunia. Bi. Shida aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, jijini Dar es Salaam amefariki dunia kwa …

Asilimia 25 ya Walimu Hufundisha ‘Makorokocho’

WAKATI Serikali ikiahidi kuboresha elimu nchini kwa kuhakikisha inaajiri walimu wa kutosha, imebainika kuwa asilimia 25 ya walimu huwafundisha wanafunzi mambo yasiyo ya msingi. Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco), iliyozinduliwa Dar es Salaam hivi karibuni, imebainisha kuwa wakati wananchi wakilalamika kuwa elimu inayotolewa haimsaidii mwanafunzi kupata ajira nzuri, wanafunzi hawajifunzi mambo ya …

Matumizi ya ARV na Pombe Hatari Hatari…!

WATU wanaokunywa dawa za kufubaza makali ya Virusi Vya Ukimwi(ARV) huku wakitumia pombe kwa wingi wametajwa kujiweka katika hatari zaidi. Wanaweza kuharibu dozi na kusababisha kushuka kwa kinga ya mwili, kuongeza kiwango cha sumu mwilini, kuharibu ini na figo. Watalaamu wa afya wanasema kuwa kiasi kidogo cha pombe kwa mtu anayeishi na VVU, hakina madhara jambo ambalo pengine limesababisha watumiaji …

Wabunge Upinzani Watoka Bungeni, Zitto Awaita Wanaroho Mbaya, Pinda Atoa Kauli ya Serikali

Na Mwandishi Wetu WABUNGE wa Kambi ya Upinzani Bungeni wametoka nje ya Bunge la Bajeti leo jioni mjini Dodoma ikiwa ni ishara ya kususia Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kwa madai hoja zao wanazowasilishwa zinapuuzwa. Wabunge hao wengi wakiwa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha Wananchi, CUF na NCCR-Mageuzi isipokuwa John Cheyo wa UDP na …

Tanzania Yafanikiwa Kupunguza vifo vya watoto…!

Na Premi Kibanga, Toronto-Canada TANZANIA imefanikiwa kufanikisha lengo la kupunguza vifo vya watoto kama yalivyoainishwa na Umoja wa Mataifa kwa juhudi za Serikali, familia na jamii kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na msaada mkubwa kutoka kwa Jumuiya ya kimataifa, washirika wa maendeleo, sekta binafsi na Mashariki binafsi mbalimbali ya kimataifa. Rais Kikwete amesema hayo tarehe 29 Mei, 2014 alipotoa hotuba …