Mtoto wa Yusuf Makamba Kugombea Urais 2015…!

NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ametangaza nia yake ya kuwania urais akisema huu ni wakati wa kupisha fikra mpya kuongoza dola, licha ya chama hicho kuzuia kutangaza nia na kupiga kampeni kabla ya muda. January Makamba ni mtoto wa mwanasiasa nguli aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za chama tawala na serikalini, Yusuf Makamba. Makamba, mmoja wa makada …

Tanzania Miongoni mwa Majeshi Bora Duniani

MAJESHI Maalum (Special Forces) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35 vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa na ufanisi wa hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa vizuri. Kwa mujibu wa Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania na jeshi lake ni …

Malkia Nomsa Matsebula Aisaidia Sekondari ya Nakayama Mil 5

Na Anna Nkinda- Maelezo MKE wa Mfalme wa Swaziland Malkia Nomsa Matsebula ameipatia shule ya Sekondari ya WAMA- Nakayama iliyopo Kijiji cha Nyamisati Wilaya ya Rufiji mkoani Pwani zaidi ya shilingi milioni tano ili ziweze kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo katika mahitaji yao ya kila siku. Malkia Matsebula ambaye ni Mke wa Mfalme Muswati alitoa fedha hizo jana wakati alipoitembelea …

Serikali Yatangaza Ajira 1,324 Nafasi Mbalimbali

SERIKALI YATANGAZA NAFASI ZA KAZI 1,324 Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania  wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,324 ambazo ni  kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini. Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi 1,334 zimeainishwa bayana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz  ili kuwawezesha …

Balozi wa Libya Ajiua kwa Risasi Ofisini…!

BALOZI wa Libya nchini Tanzania, Ismail Nwairat, amejiua kwa risasi jana ofisini kwake, katika tukio la kwanza la aina yake nchini kwa kigogo wa ubalozi kuondoa uhai wake. Hadi sasa haijafahamika sababu za kujiua kwa balozi huyo ambaye alikuwa akipingana waziwazi na sera za utawala ulioondolewa madarakani wa Kanali Muhamar Gaddafi, aliyeuawa wakati wa mapinduzi Oktoba 2011. Habari zilizopatikana jana …