Na Deogratius Temba WANAUME kutoka katika Kata ya Nyamaraga Kijiji cha Ng’ereng’ere Wilaya ya Tarime mkoani Mara wamewataka wanaume wote kukataa kuoa wasichana waliokeketwa ili kukomesha kabisa mila hizo potofu. Akizungumza katika Tamasha la Jinsia ngazi ya wilaya lililofanyika katika kata hiyo nje kidogo ya mjini wa Tarime linaloongozwa na TGNP Mtandao, Mchungaji wa Kanisa la PEFA, Getagasembe, Roberty Machera amesema …
Utajiri wa Lowassa Unavyoyatesa Makanisa Tanzania
Na Prudence Karugendo KATIKA mafundisho ya Injili, ambayo ni maelezo kuhusu Yesu Kristo, inaelezwa kwamba mama mmoja alikamatwa na kupelekwa mbele ya Kristo akituhumiwa kufanya ukahaba huku wadau waliomkamata wakimtaka Kristo kutoa hukumu ili mama huyo aadhibiwe kulingana na maelekezo ya torati. Kristo alitumia hekima yake na kusema sawa, anayejielewa ni msafi hajapata kutenda kosa la jinsi hiyo na awe …
DCB Bank Watambulisha DCB Jirani na DCB Mobile Sabasaba
DCB Commercial Bank imeendelea kuzitambulisha huduma zake mpya ikiwemo ya DCB Jirani ambayo inamuwezesha mteja wa banki hiyo kupata huduma za kibenki mahali popote kwa haraka na nafuu zaidi. Katika huduma ya DCB Jirani inamuwezesha mteja kuweka na kutoa pesa kwenye akaunti yake, kujua salio, kufungua akaunti na kupata taarifa fupi za akaunti, kutuma hela kutoka akaunti moja hadi nyingine, …
Mkataba wa Gesi Umevuja: Tanzania Kupoteza Trilioni 1.6 Kwa Mwaka
Zitto Kabwe, Mb MKATABA wa mgawanyo wa mapato yanayotokana na uzalishaji wa Gesi Asilia (PSA) kati ya Shirika la Mafuta Tanzania na Kampuni ya Mafuta ya Norway umevujishwa (https://onedrive.live.com/view.aspx?cid=0EC42B180C06D0B8&resid=EC42B180C06D0B8%21107&app=WordPdf).Toka Mkataba huo uvuje na kuanza mijadala kwenye mitandao ya kijamii, habari zake zimekuwa zinazimwa na hivyo kukosa kabisa mjadala mpana kitaifa na hasa kwa wananchi wenye rasilimali zao. Mwanzoni wengi wetu …
Papa Francis Aruhusu Wanamaombi Kanisani
MAKAO Makuu ya Kanisa Katoliki (Vatican), yametangaza kuwatambua rasmi makasisi wake wanaoombea na kutoa pepo wanaowashikilia waumini wao kama yanavyofanya makanisa ya Kipentekoste. Uamuzi huo ambao ni wa kwanza kutolewa katika historia ya kanisa hilo, umetolewa juzi na Papa Francis na kuchapishwa kwenye gazeti la Vatican la L’Osservatore Romano. Papa Francis (pichani) alibariki kundi la makasisi 250 kutoka nchi 30 …