WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema rasimu ya Sera ya Diaspora iko kwenye hatua za mwisho za maandalizi na muda si mrefu itaingizwa kwenye utaratibu wa Kiserikali ili hatimaye iweze kuwasilishwa kwenye Baraza la Mawaziri. Akizungumza na Watanzania wanaoishi Uingereza kwenye mkutano uliofanyika ubalozi wa Tanzania jijini London, mwishoni mwa wiki, Waziri Mkuu alisema mchakato wa kuandaa rasimu hiyo …
Mtanzania Mzalendo Aishauri Serikali Kuhamia Dodoma
Lorietha Laurence na Rose Masaka (SJMC) SERIKALI imeshauriwa kuendeleza mchakato wa kuhamisha ofisi zote zake mkoani Dodoma kwenye makao makuu ya nchi yetu ili kuweza kupunguza msongamano wa watu na magari. Hayo yalisemwa na Mtanzania Mzalendo, John Lyasenga wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es Salaam. “Kutokana na jiji la Dar …
JK Apongeza Vyama vya Siasa, Ashauri Viongozi wa Dini Kuombea Bunge
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amevipongeza vyama vinne vikuu vya siasa nchini ambavyo vimeanzisha majadiliano ya kutafuta namna wajumbe waliosusia Bunge Maalum la Katiba wanavyoweza kurejea Bungeni. Aidha, Rais Kikwete amewataka Watanzania kujiepusha na kishawishi cha kuingilia mchakato wa Katiba Mpya kwa maneno na kutoa kauli nyingi, nyingine zikiwa za upotoshaji na uchochezi, jambo ambalo linawanyima …
Rais Kikwete Azitaka Halmashauri Kutenga Ardhi kwa NHC
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameziagiza Halmashauri zote nchini kutenga ardhi kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa ajili ya kujenga nyumba za bei nafuu kote Nchini. Rais Kikwete ametoa maagizo hayo leo mjini Tanga wakati akifanya majumuisho ya ziara yake katika Mkoa wa Tanga. Rais amesema nyumba za bei nafuu zikijengwa zitatoa nafuu na kuondoa tatizo la makazi kwa …
Uholanzi Yawaongezea Machungu Wabrazili, Yawachapa 3-0
TIMU ya taifa ya Uholanzi imeongeza machungu kwa timu ya taifa ya Brazil katika fainali za kombe la dunia baada ya kuichapa timu hiyo mabao matatu kwa mtungi. Kipigo hicho ambacho ni cha pili mfululizo kwa wa Brazil kimetokea katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu katika fainali hizo. Timu ya Brazil katika mechi yao ya nusu fainali waliyokutana na …
Salma Kikwete Apinga Ndoa za Utotoni na Taasisi ya Segal Family
Na Anna Nkinda – Maelezo, Arusha JAMII imetakiwa kushirikiana kwa pamoja kupiga vita ndoa za utotoni hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa sera na sheria za kuwalinda watoto zinafuatwa ili watoto wa kike waweze kusoma na kumaliza masomo yao kama ilivyo kwa watoto wa kiume. Mwito huo umetolewa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akizungumza na …