Marekani Yaimwagia Lawama Misri na Falme za Kiarabu

MAOFISA nchini Marekani wamesema mataifa ya Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu zilihusika na mashambulio nchini Libya wiki iliyopita kuwalenga wanamgambo wa Kiislamu wanaopambana na vikosi vya Serikali. Ofisa mmoja Mkuu wa Marekani aliwaambia wanahabari kuwa Marekani haikushirikishwa katika mashambulio hayo na ilishangazwa. Makombora hayo yaliofyetuliwa Tripoli yanasemekana kutekelezwa na Umoja wa milki za kiarabu kwa kutumia kambi za …