WAKATI Serikali ya Tanzania imeanza kuwafikisha mahakamani baadhi ya maafisa wanaotuhumiwa kuhusika na gawio la fedha kutoka akaunti ya Tegeta ESCROW, Chama tawala nchini humo CCM, kimetoa kauli ya kuwachukulia hatua, makada wake wanaohusishwa na kashfa hiyo. Suala la kashfa ya akaunti ya mabilioni ya fedha yaliyochotwa kutoka akaunti ya Tegeta Escrow, si tu imekichafua chama tawala nchini humo kutokana …
Sakata la Escrow; Rais Kikwete Amfukuza Uwaziri Prof Tibaijuka
Na Mwandishi Wetu RAIS wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemfukuza kazia Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kwa kukiuka sheria ya maadili ya umma kwa kile kupokea kiasi kikubwa cha fedha toka kwa mfanyabiashara James Rugemalira wa VIP Engineering & Marketing. Rais alitengua uteuzi wa Waziri Prof. Tibaijuka jana alipokuwa akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar …
Bodi ya Shule Iliyopata ‘Mgao wa Escrow’ Yamtetea Prof. Tibaijuka
BODI ya Wadhamini ya Shirika la Barbro Johansson Girls’ Education Trust (JOHA TRUST au BARBRO) wamiliki wa shule za Sekondari Bingwa ya Barbro iliyopo jijini Dar es Salaam na nyingine ya Kajumulo Girls’ High School iliyopo Manispaa ya Bukoba zilizoingia katika tuhuma za kudaiwa kupata mgao wa fedha za Escrow zimetoa taarifa kumtetea Profesa Anna Tibaijuka ambaye ni mwanzilishi wa …
Wanachuo St. Joseph Waenda kwa Pinda Kudai Mgao wa Escrow
BAADHI ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yosef (St. Joseph University In Tanzania-SJUIT, Dar) wameibuka katika maandamano ya kushtukiza na kwenda hadi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakiomba nao wapatiwe mgao wa fedha za Escrow kwa ajili ya kutumia kulipia ada chuoni. Wanafunzi hao ambao walijikusanya eneo la ofisi za Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam hadi walipoondolewa …
Kashfa ya Escrow Yawagawa Wabunge Dodoma…!
TUHUMA za uchotwaji wa fedha kiasi cha bilioni 306 zinazodaiwa kuwa za Serikali katika akaunti ya Tegeta Escrow imewagawa wabunge katika mjadala unaoendelea bungeni wa kuijadili ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyowasilishwa na mapendekezo ya kutaka baadhi ya mawaziri, Waziri Mkuu na Watendaji wengine wawajibishwe. Mjadala mkali unaoambatana na vituko vya wabunge kuzomeana, kupeana vijembe, …
Serikali Yaanza Kujibu ‘Escrow’ Bungeni, Yadai PAC Imedanganya…!
SERIKALI imeanza kujibu hoja za tuhuma za uwepo wa uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow takribani sh. bilioni 306 zinazodaiwa kuchotwa na watu binafsi, viongozi wa siasa, watendaji wa Serikali pamoja na viongozi wa dini, kwa mujibu wa ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyowasilishwa jana bungeni mjini Dodoma. Akijibu hoja hizo leo mjini …