Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisalimiana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na. Serikali ya Mtaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini alipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja ya kukutana na wadau wa elimu walioshiriki mkutano wa kutathmini sekta …
TTCL Yatoa Msaada wa Compyuta 10 na Intaneti, Kusaidia Elimu
KAMPUNI ya simu Tanzania imetoa msaada wa komputa kumi pamoja na kifurushi cha internet ya bure yenye kasi ya 2Mbps kwa muda wa miezi sita kwa kituo cha Global Outreach Tanzania vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni ishirini laki moja na tisini na saba elfu mia sita ( Tshs.20, 197,600/=) ili kuendeleza juhudi zinazofanywa na Serikali na wadau wengine …
Mpango wa Kukuza Stadi za Kusoma Wazinduliwa, KKK
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amezindua Mpango wa Kitaifa wa Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaolenga kukuza viwango vya uelewa kwa watoto wa darasa la kwanza na la pili kwa nchi nzima. Mpango huo wa miaka mitatu ulioanza kutekelezwa 2014/2015 hadi 2016/2017 umelengwa kuwahusisha watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 13 walio kwenye mfumo rasmi …
HakiElimu Yakosoa Mpango wa BRN Sekta ya Elimu
Na Joachim Mushi TAASISI ya HakiElimu imeukosoa mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ‘Big Results Now’ (BRN) unaotekelezwa na Serikali katika sekta nyeti ikiwemo elimu kwa madai kuwa matokeo yake kwenye sekta ya elimu sio ya kuridhisha. Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya tathmini …
Tanzania Yatolewa Mfano Kutekeleza Mpango wa Elimu wa EFA
Na Mwandishi Wetu TANZANIA imekuwa moja wapo ya nchi za kutolea mfano miongoni mwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara katika kutekeleza maazimio ya mpango wa Elimu kwa wote (EFA). Akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa wadau wote wa elimu , Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi nchini Tanzania Mh. Dkt. Shukuru Kawambwa amesema Tanzania …
CIP Trust Yatumia Mil 16 Ujenzi wa Madarasa, Ofisi Shule ya Kata
Na Nathaniel Limu, Singida SHIRIKA lisilo la kiserikali la Community Initiatives Promotion Trust Fund (CIP Trust), limetumia zaidi ya shilingi 16 milioni, kugharamia ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu, katika shule ya msingi Kinyamwenda kata ya Itaja. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la CIP Trust, Affesso Ogenga, wakati akitoa taarifa ya ujenzi huo kwenye …