Kamati ya Rufaa TFF Yamjadili Dk Ndumbaro

KAMATI ya Rufaa ya Nidhamu – TFF imekutana leo tarehe 12/04/2015 kujadili rufaa No. 1/2014 ya DR. DAMAS  NDUMBARO dhidi ya TFF. TFF iliwakilishwa na Wakili Msomi Emmanuel Muga na Dr. Ndumbaro hakufika wala hakuwakilishwa na wakili wake.   Kufuatia kutofika kwa Dr. Ndumbaro, Kamati, kwa Azimio moja, iliamuru TFF itoe wito mpya na  mpaka tarehe 14/04/2015 uwe umemfikia Dr. …