Dk. John Pombe Magufuli Aapishwa Kuwa Rais wa Tanzania

  Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akionesha mkuki na ngao kama ishara ya mamlaka mara baada ya kula kiapo leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.   Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia) akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande leo katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. …

Dk Magufuli Atema Cheche, Kuanza na Watendaji Serikalini

RAIS mteule wa Tanzania anayesubiri kuapishwa, Dk. John Magufuli amewataka wantendaji wa Serikali wasiopenda kujituma, wazembe na wavivu waanze kujipanga kwani katika utawala wake hawezi kuwavumilia atafukuza mmoja baada ya mwingine na kubaki na wanaotaka kufanya kazi kwa kujituma. Dk. Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam akizungumza kutoa shukrani kwa baadhi ya wananchi na WanaCCM waliofika kwenye …

NEC Yamkabidhi Dk Magufuli Hati ya Kuteuliwa Urais

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imewakabidhi rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli pamoja na Makamu wa Rais mteule, Mama Samia Suluhu Hassan hati za uteuzi kushinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015. Hafla ya kukabidhiwa hati hizo umefanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa …