Rais Zuma Ateta na JK Ikulu, Dk Bilal Amsindikiza
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya Desemba 22, 2014, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma. Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, yalichukua kiasi cha saa moja na dakika 45 na yalihusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Rais Zuma ambaye aliwasili nchini usiku wa Desemba 21, 2014, …
Dk Bilal Awahutubia Wawakilishi Mkutano wa Mazingira Afrika
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal Desemba 10, 2014, amewahutubia wawakilishi wa Afrika katika Mkutano wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, nchini Peru. Mheshimiwa Makamu wa Rais anahudhuria mkutano huu akimuwakilisha Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Kiongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi. Mkutano huo …
Dk Bilal Amwakilisha JK Mkutano wa Kimataifa wa Mazingira Duniani
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal Desemba 09, 2014 amemuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni Mwenyekiti Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali Barani Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, kwenye mkutano wa Kimataifa wa Mazingira Duniani (Cop20) unaofanyika jijini Lima, Peru. Pamoja na shughuli nyingine ambazo zimemuhusisha Makamu wa Rais …