Mtambo huu ni sehemu ambapo maji huendelea kusafishwa na kisha kupelekwa katika mtambo maalum wa kukusanya na kusafirisha kwenda kwa wananchi. Matanki makubwa ya maji yenye mitambo maalum ya kusafisha maji kama inavyoonekana hapa maji yakiendelea kusafishwa. Sehemu hii ni ya mtambo ambapo maji yanawekwa dawa na kisha kupelekwa katika sehemu ya mtambo mwingine kwa ajili ya …
DAWASCO Yakanusha Gari Lao Kusababisha Ajali Namanga Oysterbay
Na Mwandishi Wetu, SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), imekanusha taarifa iliyoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya gari linalodaiwa kuwa la DAWASCO lenye namba za usajili T 369 BUZ ambalo liliparamia kituo cha mabasi cha Mbuyuni kilichopo maeneo ya Namanga Oysterbay na kujeruhi watu watatu. Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Meneja uhusiano wa Dawasco, Bi. Everlasting Lyaro …
DAWASCO Kuzima Mtambo wa Maji wa Ruvu Chini
KUZIMWA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU CHINI SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO), LINAWATANGAZIA WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI KUWA, MTAMBO WA KUZALISHA MAJI WA RUVU CHINI UTAZIMWA KWA SAA 36 KWA SIKU YA ALHAMIS TAREHE 18.02.2016. KUZIMWA KWA MTAMBO HUO KUMETOKANA NA MATENGENEZO KATIKA BOMBA KUU LENYE UKUBWA WA INCHI 54 LINALOSAFIRI MAJI KUTOKA …
DAWASCO Yakanusha Kusambaza Maji ya Kinyesi
KAIMU Meneja Uhusiano wa Dawasco, Everlasting Lyaro amekanusha kampuni hiyo kuhusika katika usambazaji maji yanayodaiwa si salama na kuwa na vimelea vya wadudu (kinyesi). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam. Mnamo tarehe 08/11/2015 Magazeti ya Mzalendo na Majira yaliandika habari zilizolenga upotoshaji na taharuki kwa wananchi na hususa ni watumiaji wa Maji kwa …