David Cameron Ashinda Uchaguzi, Mpinzani Wake Ajiuzulu

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo jana. Chama chake cha Conservative kimepata viti 330 huku kile cha leba kikijipatia 232. Cameron alisema anapania kuendelea kuiongoza Uingereza kwa umoja. Shirika La BBC lilikisia kuwa Cameron na Chama chake angepata ushindi wa maeneo bunge 329. Chama cha Leba kimepata pigo kubwa huko Scotland …