Maandalizi ya Kusheherekea Miaka 50 ya Muungano

Pichani juu, Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni zikiwa zimepambwa kwa bendera ya Tanzania, sambamba na maeneo mengine ya Jiji la Dar. Wakati mabilioni yakitumika kuandaa sherehe za Muungano, hoja na kejeli ziliendelea kutikisa (na bila shaka zitaendelea pindi wajumbe watakaporudi tena Dodoma Agosti mwaka huu) kuhusu muundo stahiki wa muungano. Serikali moja, mbili au tatu!? Picha Zote na …

Bustani ya Kupumzikia Yageuzwa Makazi!

Pichani, ni eneo la Umoja Wa Vijana, Mtaa wa Kipande karibu na Exim Bank, inaonekana nguo zikiwa zimeanikwa kwenye Bustani hiyo au kwa ung’eng’e Park. Kwa mbaliii, anaonekana kijana akiwa ameuchapa usingizi chini ya viti vya bustani. Your browser does not support the video tag Video hii, kijana anaonekana akikojoa nyuma ya benchi la Bustani. Kwa mtaji huu, bustani hii …

Wakazi wa Jangwani Waanza Kurejea Kwenye Makazi Yao Licha ya Maafa Yaliyowakuta!

Kama picha zilivyonaswa na thehabari hapo juu, inaonekana wakazi wa Jangwani wakirejesha makazi yao licha ya maafa makubwa yaliyowakuta kutokana na mvua kubwa zilizolikumba jiji la Dar hivi karibuni. Magodoro na vifaa mbalimbali vilionekana vikiwa vimeanikwa juu ya mapaa na kwingineko, tayari kuanza maisha mapya. Inasemekana serikali iliwahamishia wakazi hao eneo la Mabwepande, Manispaa ya Kinondoni, lakini inaonekana baadhi yao …

Mafuriko Ya Dar Yaleta Neema Kwa Baadhi ya Wakazi Wake!

Thehabari leo ilivinjari maeneo ya Mto Mzinga, eneo la kwa Mpalange, Manispaa ya Temeke, na kushuhudia biashara ya kuvusha watu ikiendelea kutoka upande mmoja wa Maji Kwenda mwingine. Pichani,wanafunzi (watoto)wakiwa wamebebwa na watoa huduma. Thehabari iliweza kugundua kwamba watu wazima hutozwa shillingi 500 ili kuvushwa. Uvushaji ukiendelea Wakati huo huo, vijana wengine wamebuni ajira ya kujikusanyia mchanga unaopatikana oembezoni mwa …

Je Huu ni Usafiri Kafiri Au..?

Pichani, ni wakazi wa jiji la Dar es Salaam kama walivyonaswa leo na mpiga picha wetu wakiwa kwenye heka heka za kuingia kwenye Daladala, ambalo lipo kimitego mitego kama picha inavyojionesha hapo juu. Picha hii inaonesha kidumu cha mafuta kikiwa kimefungwa kiaina (kienyeji) kutokea kwenye injini ndani ya basi la abiria. Hivi bahati mbaya ukija kutokea mlipuko ndani ya daladala …