MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq ametoa tahadhari kwa wakazi wa jiji hilo kuwa makini kwani ugonjwa wa kipindupindu tayari umevamia baadhi ya maeneo ya jiji. Mkuu huyo wa mkoa alisema tayari watu 24 wamelazwa baada ya kubainika kuwa na ugonjwa huo, huku watu wengine wawili (mwanamke na mwanaume) wameshapoteza maisha kwa ugonjwa huo. Alisema taarifa …
Polisi Kutoa Milioni 50 kwa Atakayetoa Taarifa Uvamizi Stakishari…!
JESHI la Polisi limetangaza kutoa kiasi cha shilingi milioni 50 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa sahihi juu ya wavamizi wa Kituo cha Polisi Stakishari kilichopo eneo la Ukonga ambao waliuwa raia na askari wanne kabla ya kupora baadhi ya silaha kituoni hapo. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es …
Polisi Wadhibiti ‘Majambazi’ Mtaa wa Samora na Nkruma Dar
Kijana mwingine anayedaiwa kuwa ni jambazi akiwa amekamatwa. Watuhumiwa hao wanne wa ujambazi wakiwa ndani ya Noah kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi. Kulia ni askari Polisi. Askari kanzu (katikati), ndiye anadaiwa kuwadhibiti majambazi hayo kabla ya kujificha chini ya uvungu wa taxi zinazoegeshwa jirani na Mnara wa Saa katika makutano ya barabara ya Uhuru, Samora na Nkruma. Gari …
Hospitali za Apollo Kuokoa Zaidi ya Watu 100 Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Dar
HOSPITALI za Apollo zimekuwa mstari wa mbele kwa teknolojia ya hali ya juu na zinaongoza katika kutoa huduma nafuu za matibabu kwa wagonjwa duniani kote. Apollo wanashiriki kwenye Maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa mara ya kwanza. Hospitali za Apollo ziko hapa kutangaza huduma wanazotoa na kuongeza uelewa kuhusu Apollo. Wageni mbalimbali wanaotembelea Saba …
Sababu za Mafuriko Kila Sehemu Dar es Salaam Zatajwa
MVUA zinazoendelea kunyesha nakusababisha mafuriko na hasara kubwa jijini Dar es Salaam na maeneo mengine nchini zimetajwa kuwa ni moja ya ushahidi wa udhaifu wa miundombinu ya kweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo ni janga kubwa duniani kwa sasa. Haya yalisemwa na FORUMCC; shirika linalijihusisha na masuala ya mabadiliko ya Tabianchi. Watu zaidi ya 12 wameripotiwa kupoteza maisha mpaka sasa kutokana mafururiko hayo …