Lowassa Apanda Daladala Toka Gongo la Mboto hadi Pugu

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Lowassa …

Auawa Baada ya Kuwachoma Visu Abiria Kwenye Daladala

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Mosha Mahona ameuawa na wananchi baada ya kuwachoma kwa kisu abiria watano waliokuwa kwenye daladala linalofanya safari zake kati ya Posta na Ubungo Simu 2000. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa moja usiku katika eneo la Magomeni Usalama na Mahona aliuawa kwa kushambuliwa na …

Madereva Wetu Ndio Husababisha Misongamano Isiyo ya Lazima Barabarani!

Picha zinaonyesha magari (mara nyingi Daladala) yakiendeshwa upande wa gari zitokazo upande wa pili, maarufu kama “Kutanua”! Tabia hii imekuwa ikisababisha misongamano, isiyokuwa ya lazima kwenye barabara zetu za Dar. Nidhamu ya matumizi ya barabara imetoweka kabisa Tanzania, sijui tunaelekea wapi? Ajali zinachukua maisha ya watu na mali Kila kukicha. Picha hizo zimenaswa kwenye barabara itokayo Tandika kwenda Buza, maeneo …

Wito Kwa Kina Baba Kuondoa Dhana Potofu!

Maisha ya sasa kushirikiana kama picha zinavyoonyesha hapo juu, mke na mume kwakishirikiana kuuza vitumbua. Mke akichoma na mume akiwa anatoa huduma kwa wateja, ambao hujitokeza kwa wingi mida hii ya asubuhi pale maeneo ya “Davis Corner”, Tandika, Manispaa ya Temeke katika kituo cha daladala ziendazo Abiola na Buza kanisani. Kitumbua kimoja huuzwa kwa Tsh 100, na awali kabla ya …

Mwananchi- Usifikiri Dampo, ni Kituo Cha Daladala!

Picha ya kwanza, inaonyesha chakula (mapaja ya kuku) kikiuzwa pembezoni mwa kituo cha Mabasi, Banana, wilayani Ilala. Meza zimewekwa juu ya mifereji ya kupitisha Maji ya mvua, ambayo nayo imejaa taka za aina mbalimbali. Picha ya pili ni wakazi wakipita kwa taabu juu ya Maji yenye kinyesi, baada ya baadhi wa wananchi kutumia fursa hii ya mvua kutapisha vyoo! Picha …