Pinda Aridhishwa na Ujenzi Miundombinu OUT

  WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amesema uamuzi wa Serikali wa kukopa fedha ili kuboresha miundombinu kwenye taasisi za elimu ya juu nchini ulichukuliwa kwa lengo la kujibu tatizo la sasa la wingi wa vijana wanaohitimu kidato cha sita.   Ametoa kauli hiyo Oktoba 10, 2014 wakati akizungumza na wahadhiri, wakufunzi, wanafunzi na wanajumuiya ya Chuo Kikuu Huria (OUT) …