Wanafunzi wa Awali Tunduru Wasomea Chini ya Mti

Na Joachim Mushi, Tunduru WANAFUNZI wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wanasomea chini ya mti kutokana na darasa hilo kuendeshwa bila ya kuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusomea wanafunzi hao. Hali hiyo imebainika baada ya mwandishi wa habari hizi kuitembelea shule hiyo hivi karibuni na kuwakuta wanafunzi wakiwa wamekaa chini …