China Yatoa Mabilioni ya Fedha Kuwekeza Miradi Anuai Tanzania

*Maendeleo ya China ni Cachu….! TANZANIA na Jamhuri ya Watu wa China Oktoba 23, 2014, zimetiliana saini Hati za Makubaliano (Memorandum of Undestanding) ambako taasisi za China zitawekeza mabilioni ya dola za Marekani katika uchumi wa Tanzania. Shughuli hiyo ya utiaji saini imekuwa sehemu ya Mkutano wa Tatu wa Uwekezaji Kati ya Tanzania na China uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano …

JK Afagilia Kiwango cha Uwekezaji China

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kuwa anafurahishwa na kiwango cha uwekezaji wa makampuni ya Jamhuri ya Watu wa China katika uchumi wa Tanzania ambao hadi mwishoni mwa mwaka jana ulikuwa umefikia miradi 522 yenye thamani ya dola za Marekani 2,490.21 milioni (dola bilioni 2.5). Rais Kikwete amesema kuwa kiwango hicho kinaufanya uwekezaji wa China katika …

Rais Kikwete Aanza Ziara Rasmi ya Kikazi China

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete Oktoba 21, 2014, anaanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping, ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Baada ya China, Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Vietnam kwa mwaliko wa …