Nishati na Madini Kufadhili Masomo Nchini China
Mwanahabari Salome Kitomari kutoka gazeti la Nipashe, akiuliza maswali katika mkutano huo. Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo. Hapa mkutano ukiendelea. Na Dotto Mwaibale WIZARA ya Nishati na Madini imetangaza nafasi za masomo kwa vijana wa Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Watu wa China kwa kipindi cha mwaka 2015. Hayo yalibainishwa na Msemaji wa Wizara hiyo …
Tanzania Yaomba Msaada wa Madaktari Kutoka China
*Yashukuru ujenzi hospitali ya magonjwa ya moyo TANZANIA imeiomba Jamhuri ya Watu wa China kuongeza idadi ya madaktari wake inaowatuma Tanzania kama msaada kutoa huduma ya tiba kama njia ya kuzidi kusaidia kukabiliana na upungufu wa madaktari nchini. Aidha, Tanzania imeishukuru China kwa kujenga hospitali kubwa inayoweza kulaza wagonjwa 100 kwa wakati mmoja wa magonjwa ya moyo na yenye uwezo …
China Kupeleka Dola Milioni 85 Kusaidia Mapambano ya Ebola
JAMHURI ya Watu wa China Oktoba 24, 2014 imetangaza kuwa kwa mara ya nne katika kipindi kifupi inapeleka msaada wa dawa, vifaa na mahitaji mengine ya tiba yenye thamani ya dola za Marekani milioni 85 kukabiliana na ugonjwa wa Ebola kwa nchi tatu za Afrika Magharibi ambazo zinapambana na ugonjwa huo ambao mpaka sasa umeua zaidi ya watu 4,000. Aidha, …
China ‘Yamwaga’ Mabilioni Miradi ya Maendeleo Tanzania
JAMHURI ya Watu wa China, Oktoba 24, 2014, imetangaza neema kubwa kwa Tanzania, ikiwa ni pamoja na kutoa dola za Marekani milioni 85 kwa ajili ya shughuli za maendeleo na kuisaidia Tanzania kufanya mageuzi ya viwanda. Neema hiyo ya China kwa Tanzania imetangazwa na Rais Xi Jinping wa nchi hiyo katika mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati yake na ujumbe wa …
- Page 1 of 2
- 1
- 2