JK Atuma Salam za Rambirambi kwa Chifu Mkwawa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Chifu Abdu Adam Mkwawa, ambaye aliaga dunia jana, Jumamosi, Februari 14, 2015 hospitalini mjini Iringa. Katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza Februari 15, 2015, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na kushtushwa na kifo cha Chifu Mkwawa ambaye amemwelezea …