Vijana Marafiki wa Lowassa Dar Wahamia Chadema

Na Mwandishi Wetu BAADHI ya vijana wa kundi la 4U Movement waliokuwa wakimuunga mkono Edward Lowassa leo wamerudisha kadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Akizungumza na mtandao huu mmoja wa wawakilishi wa vijana hao, Michael Litanda alisema takribani vijana 100 waliokuwa katika kundi hilo la 4u Movement wameamua kukihama Chama Cha …

Mwenyekiti Chadema Moshi Vijijini Ajiandikiza Kupiga Kura

Kiwia akijaza moja ya fomu zinazotakiwa kujazwa wakati wa zoezi a uandikishwaji. Mtia nia wa nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi Vijijini, Evarist Kiwia akichukuliwa Taswira kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho maalumu kwa ajili ya kupigia kura. Kiwia akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo mpya wa BVR. …

Freeman Mbowe, Ndesamburo Wanguruma Kilimanjaro…!

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Jafary Michael akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway mjini Moshi. Mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini, Philemon Ndesamburo walipokutana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Railway mjini Moshi, wengine ni Mwenyekiti wa …

Zitto Kabwe Njiapanda, Chadema Wamfukuza

HALI ya kisiasa ya mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe imewekwa njiapanda baada ya Chadema kutangaza kumvua uanachama saa chache baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi aliyofungua dhidi ya chama hicho kikuu cha upinzani. Zitto, ambaye amedumu kwenye nafasi ya ubunge kwa takriban mwaka mmoja kutokana na amri ya mahakama, sasa atalazimika kuamua kutangaza rasmi kujiunga na chama kipya …

Breaking Newz; Mbowe Ashinda Tena Uenyekiti CHADEMA

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefanikiwa kutetea nafasi yake tena ya kukiongoza chama hicho baada ya kushinda katika uchaguzi wa chama hicho uliyofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mlimani City. Kwa mujibu wa taarifa ambazo mtandao huu umezipata kutoka katika eneo la uchaguzi, Freeman Mbowe ametwaa kiti hicho tena baada …

CHADEMA Yamshukuru Rais Kikwete, Yeye Ataka Wananchi Wasitumike Chambo

Na Mwandishi Maalumu, Karatu CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete kwa kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Wilaya ya Karatu katika Mkoa wa Arusha. Aidha, chama hicho kimempongeza Rais Kikwete kwa kusambaza maendeleo kwa Watanzania bila kujali msimamo wao wa kisiasa na hata katika maeneo yanayounga mkono upinzani. Shukurani na …