Kiongozi wa Upinzania Auwawa Burundi

KIONGOZI wa chama kidogo cha upinzani nchini Burundi ameuawa kwa kupigwa risasi. Mwili wa kiongozi huyi, Zedi Feruzi pamoja na wa mlinzi wake ulipatikana nje ya nyumba yake kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Bujumbura. Mauaji ya mwanasiasa huyo yanafanyika wakati wanaharakati wa upinzani nchini humo wamesitisha kwa siku mbili maandamano yao dhidi ya Rais Pierre Nkurunziza kupinga uamuzi wake …

Jeshi Linalomtii Rais Nkurunziza Lazima ‘Mapinduzi’ Burundi

JESHI linalomtii Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza jana lilifanikiwa kuzima mapinduzi ya kijeshi yaliyopangwa kufanywa na wanajeshi wafuasi wa Meja Jenerali Godefroid Niyombare aliyetangaza kupitia kituo kimoja cha redio kuwa ameipindua serikali ya Nkurunzinza. Jeshi linalomtii Rais Nkurunziza limesema tayari limeweka ulinzi katika makazi ya rais na limetoa masaa sita kwa wanajeshi wafuasi wa Meja Jenerali Niyombare wajisalimishe kabla ya …

Mwenyekiti Vuguvugu la Maandamano Burundi Azungumza Tanzania

 Mwenyekiti wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni mwanaharakati wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau.  Hapa mwanaharakati huyo akisisitiza jambo kwa wanahabari. Salha MohamedMWENYEKITI wa Chama cha UPD-Zigamimbaga, ambaye pia ni Mwenyekiti wa vuguvugu la maandamano nchini Burundi, Mugwengezo Chauvineau, amewataka viongozi wa nchi za Afrika Mashariki kutokubaliana na maamuzi ya raisi Pierre Nkurunzinza kuwania kiti cha urais …

JK: Salama ya Burundi ni Kuheshimu Katiba na Sheria

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), amewashauri viongozi na wananchi wa Burundi kufanya mambo manne muhimu ili kutuliza hali ya sasa ya kisiasa katika nchi hiyo na hivyo kuepusha ukosefu wa utulivu wa kisiasa na hata kuzuka kwa machafuko. Rais Kikwete …

Uainishaji Mipaka Kimataifa Burundi na Tanzania Hauwagawi wakazi

Na Aron Msigwa – MAELEZO, Kagera MARAIS wa Tanzania na Burundi wamewatoa hofu wakazi wa maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Burundi kuwa zoezi la Uimarishaji mpaka wa kimataifa kati ya nchi hizo linalofanywa na wataalam wa upimaji na ramani katika maeneo ya mipaka ya nchi hizo halilengi kuleta mgawanyiko miongoni mwao bali kuweka utaratibu mzuri wa utambuzi wa alama za …