TAASISI ya Misaada ya Kijamii ya Hamisi Kigwangalla inayomilikiwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla imejitolea kumlipia ada mtoto Getrude Clement kwa kumsomesha kidato cha tano na sita ikiwa ni kutambua mchango wa mtoto huyo kuliwakilisha taifa. Uamuzi huo wa kumsomesha Getrude umekuja baada ya mtoto huyo kukaribishwa kuzungumza kwenye kikao …
Bajeti ya Serikali Yapitishwa Rasmi Bungeni
BAJETI ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016, imepitishwa na Bunge, huku kwa mara ya kwanza Mbunge wa Vunjo Augustine Mrema akiipinga, lakini wabunge watatu wa upinzani waliiunga mkono. Akitangaza matokeo hayo, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema bajeti hiyo ilipita kwa asilimia 83 baada ya kupigiwa kura za ndiyo na wabunge 219. Dk Kashililah alisema jumla ya …
Zitto Kabwe Akubali Kung’atuka Bungeni, Atoa ya Moyoni…!
Hotuba ya ZITTO KABWE Aliyotaka Kuitoa Bungeni Jana Mheshimiwa Spika, nilijiunga na Bunge lako tukufu mwaka 2005 nikiwa kijana mdogo mwenye malengo ya kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusu nchi yetu na pia kutetea maslahi ya wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma. Katika kudumu kwangu kama mbunge nililelewa na kukuzwa na chama cha siasa cha …
Maagizo ya Waziri Mkuu Pinda Yaendelea Kufanyiwa Kazi na Polisi!
Miezi kadhaa iliyopita waziri Mkuu Pinda alitoa maagizo wakati anazungumza bungeni kwamba Watanzania wataokuwa wanaandamana “wapigwe tu”. Tokea agizo hilo litolewe na mkuu huyu, polisi wetu wameendelea kuwa wakatili na wanyama dhidi ya Watanzania wenzao kwa kisingizio kwamba wanavunja sheria. Mimi sio hakimu, na wala sitaki kuingia kwenye mjadala kwamba wamevunja sheria au lah! Tatizo ninalo liona hapa ni uvunjaji …
Serikali Yaanza Kujibu ‘Escrow’ Bungeni, Yadai PAC Imedanganya…!
SERIKALI imeanza kujibu hoja za tuhuma za uwepo wa uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow takribani sh. bilioni 306 zinazodaiwa kuchotwa na watu binafsi, viongozi wa siasa, watendaji wa Serikali pamoja na viongozi wa dini, kwa mujibu wa ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyowasilishwa jana bungeni mjini Dodoma. Akijibu hoja hizo leo mjini …
Polisi Wawapiga Mabomu ya Machozi Wabunge Bungeni
POLISI wa Mji Mkuu wa Lagos, nchini Nigeria, wamefyatua gesi ya kutoa machozi ndani ya Jengo la Bunge, na kulazimisha kuahirishwa kwa mjadala muhimu wa bunge hilo kuhusu kurefushwa kwa kipindi cha hali ya tahadhari Kaskazini mwa nchi hiyo. Taarifa za mwaandishi wa habari hizi inaeleza kuwa maofisa wa Polisi walikuwa wakijaribu kumzuia Spika wa Bunge la Wawakilishi, Aminu Tambuwal …
- Page 1 of 2
- 1
- 2