Umoja wa Azaki za Vijana Watinga Bunge la Katiba

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma UMOJA wa Azaki za Vijana wakutana na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta wakiwa na lengo la kuja kuwasilisha mapendekezo yao kwa ajili ya maboresho ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya. Akizungumza kwa niaba ya vijana wenzake, Kiongozi wa msafara huo Alfred Kiwuyo amesema kuwa Azaki hizo za vijana zilishiriki mchakato mzima wa …

Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Waunga Mkono Bunge la Katiba

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mzumbe cha Morogoro wameunga mkono mchakato wa Bunge Maalumu la Katiba wakisema kuwa wanaridhishwa na hatua iliyofikiwa na mwendo mzima wa Bunge hilo na kuwa mwafaka unawezekana kuhusu vipengele viliyobakia na kupatikana kwa theluthi mbili za kupitisha Katiba Mpya. Wanafunzi hao wameeleza msimamo wao huo, Agosti 25, 2014, chuoni hapo kwenye risala ambayo wameisoma hadharani …

Maandalizi ya Kusheherekea Miaka 50 ya Muungano

Pichani juu, Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni zikiwa zimepambwa kwa bendera ya Tanzania, sambamba na maeneo mengine ya Jiji la Dar. Wakati mabilioni yakitumika kuandaa sherehe za Muungano, hoja na kejeli ziliendelea kutikisa (na bila shaka zitaendelea pindi wajumbe watakaporudi tena Dodoma Agosti mwaka huu) kuhusu muundo stahiki wa muungano. Serikali moja, mbili au tatu!? Picha Zote na …

Siku 67 za Mipasho, Matusi Bungeni Zamalizika..!

BUNGE Maalumu la Katiba linaahirishwa leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata ibara moja kati ya 240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba. Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta “Mzee wa Kasi na Viwango” linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu likiendelea kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi …

Sitta Amwita Bungeni Lukuvi, Aeleze Alichokisema Kuwaudhi UKAWA

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amemwita katika bunge hilo Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi aje kueleza alichokisema katika kanisa moja juzi, kauli ambayo inadaiwa kuwaudhi wabunge toka Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao ni wajumbe wa Bunge la Katiba waliogoma kuhudhuria vikao vya bunge hilo tangu jana. …

Wabunge 200 Wasusia Bunge la Katiba, Watoka Ukumbini…!

MAMBO yamebadilika. Ukimya ulitawala jana katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge zaidi ya 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia vikao vya Bunge hilo. Ilikuwa ni saa 10:31 jioni baada ya Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipohitimisha uchangiaji wake akisema: “Ukawa hatuwezi kuendelea kushiriki …