Luteni Kanali Issac Zida Kuiongoza Bukina Faso

LUTENI Kanali Issac Zida amechaguliwa na viongozi wa Jeshi la Bukina Faso kuiongoza nchi hiyo kuelekea katika taratibu za kufanya uchaguzi. Baada ya kutoka kwa maamuzi hayo ya Jeshi sasa yameondoa sitofahamu iliyokuwepo ya kwamba ni nani atakaye mrithi Rais Blaise Campaore ambaye alijiuzulu kwa nguvu za wananchi kufuatia maandamano ya kumpinga yalioambatana na vurugu kubwa. Luteni Kanali Zida tayari …

Mambo Yaharibika Bukina faso Jeshi Lapindua Nchi

AMIRI Jeshi Mkuu wa Jeshi la Burkina Faso, Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge la nchi. Kiongozi huyo mkuu wa jeshi hata hivyo hakuweka wazi ni nani atakayeshikilia uongozi wa taifa hilo kwa sasa. Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi aliyepinduliwa …

Waandamanaji Bukina faso Wachoma Bunge Kumpinga Rais

WANANCHI wa Bukina Faso wanaoendeleza maandamano wameteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, ikiwa ni hatua ya kupinga kuongeza muhula wa kutawala kwa Rais Blaise Compaore wa nchi hiyo ambaye ametawala nchi kwa miaka 27. Vituo vya Televisheni ya Taifa navyo vililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji hao kuvamia majengo ya shirika la utangazaji. Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais huku …

Wananchi Bukina Faso Waandamana Kumpinga Rais

KUMETOKEA vurugu kubwa baina ya maelfu ya waandamanaji na maofisa wa polisi katika Mji Mkuu wa Burkina Faso, Ougadougou wakati maelfu ya raia wa nchi hiyo walipokuwa wakihudhuria mkutano kupinga marekebisho ya Katiba itakayomruhusu rais wa nchi hiyo, Blaise Compaore kuongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano. Maofisa wa usalama walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya wanadamanaji hao …