Bondia Fadhili Majiha Apigwa Thailand, Alalamikia Waamuzi…!

Na Mwandishi Wetu BONDIA wa uzito wa ‘Bantamweight’, Fadhili Majiha ‘Stoper’ mwishoni mwa wiki alikuwa na kibarua kizito kutoka kwa bondia wa Thailand, Pungluang Sor Singyu aliyemenyana naye nyumbani kwao Thailand na kupigwa kwa pointi. Akizungumzia matokeo hayo, Stoper amejinasibu kuwa alipaswa kushinda pambano hilo kwani alicheza kwa umakini mkubwa lakini waamuzi walimpendelea mpinzani wake kwa kuwa alikuwa akicheza nyumbani. …