Vifo vya bomu Nigeria vyafikia 118

Maafisa nchini Nigeria wamesema kuwa wamepata maiti 118 kufuatia shambulio la bomu katika mji wa Jos. Mabomu mawili yalilipuka mojawepo ikiwa imefichwa ndani ya gari na kulipuka katika soko moja kubwa. Dakika 20 baadaye mlipuko wa pili ulitokea karibu na hospitali. Inahofiwa kuwa kuna maiti zaidi zilizonaswa kwenye vifusi vya majengo yaliyo poromoka kutokana na shambulio hilo. Kufikia sasa hakuna …