Boko Haramu Wasababisha Uchaguzi Kuahirishwa

MKUU wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, Attahiru Jega, amesema upigaji kura hauwezi kufanyika nchini humo Jumamosi ijayo kwa sababu wanajeshi wanaotakiwa kulinda vituo vya kupigia kura wanatumika kupambana na kundi la Boko Haram. “Hatari ya kutumia vijana wetu katika jeshi na kuwataka watu watumie haki yao ya kidemokrasi, katika hali ambapo hawawezi kuhakikishiwa usalama wao, ndio jukumu letu kubwa. …

Boko Haram Wateka Kambi ya Jeshi Nigeria, Shahidi wa ICC Afariki

MAOFISA nchini Nigeria wamesema kuwa kundi la Boko Haram limeuteka Mji na kambi moja ya kijeshi inayotumiwa na wanajeshi wa kimataifa wanaojaribu kukabiliana na wapiganaji hao. Seneta wa Borno Kazkazini Maina Ma’aji Lawan, eneo la Mji wa Baga amesema kuwa wanajeshi waliitoroka kambi yao baada ya kushambuliwa na Boko Haram jumamosi asubuhi. Wakaazi wa Baga, ambao walitoroka kupitia maboti hadi …

Islamic State Wamuua Kinyama Mmarekani, Boko Haram Watimuliwa Chibok

KANDA moja ya video iliowekwa mtandaoni inaonesha mauaji ya kinyama mfanyakazi wa huduma za misaada raia wa Marekani, Abdul Rahman Kassig ambaye anajulikana kama Peter Kassig kabla ya kutekwa nyara na wanamgambo wa Islamic State nchini Syria mwaka uliopita. Video hiyo inamuonyesha mawanamume mmoja anayeonekana kuwa mwanachama wa Islamic State akiwa na kisu mkononi na maandishi yanayosema kuwa Peter Kassig …

Boko Haram Wateka Vijiji Wauwa, Nigeria Hakuna Ebola…!

WATU wanaohisiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram, wamewapiga risasi na kuwachinja watu katika vijiji vitatu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria licha ya serikali kudai mwishoni mwa wiki kuwa ilifikia makubaliano na kundi hilo. Wapiganaji wa Boko Haram, walivamia vijiji viwili Jumamosi na kupandisha bendera yao kwa mara ya tatu. Hii ni kwa mujibu wa wanakijiji wa eneo hilo. Serikali ilisema kuwa …

Boko Haram Kuwaachia Wasichana Iliowateka

SERIKALI ya Nigeria imesema kuwa imefikia makubaliano na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kuhusu kuachiwa kwa wasichana waliotekwa nyara wa kutoka Chibok. Mkuu wa Jeshi la Nigeria, Alex Badeh aliyefichua makubaliano hayo mwishoni mwa mkutano wa siku tatu kati ya nchi hiyo na Cameroon ambapo alisema kuwa wanajeshi wa Nigeria watatimiza matakwa ya makubaliano hayo kabla ya kuachiwa kwa …

Boko Haram Kuwauza Wasichana Iliyowateka, Polisi Watumia Fedha Kuwasaka

KUNDI la Boko Haram limekiri kuwateka nyara wasichana wa shule moja nchini Nigeria na limesema kuwa linajiandaa kuwauza. Polisi nchini Nigeria wameahidi kumtunuku dola laki tatu za marekani yeyote atakayetoa habari zitakazowasaidia kuwapata zaidi ya wasichana mia mbili waliotekwa na kundi la wapiganaji wa boko haram mwezi uliopita. Juma lililopita wapiganaji wa Boko Haram walisema kuwa wasichana hao 200 kutoka …