JK Amteuwa Samwel Shelukindo Kuwa Balozi na Msaidizi Wake

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amemteua Samwel William Shelukindo kuwa Balozi na pia kuwa Msaidizi wa Rais (Diplomasia). Kabla ya uteuzi huu, Samwel William Shelukindo alikuwa Mkuu wa Utawala kwenye Ubalozi wa Tanzania Mjini Addis Ababa Ethiopia. Uteuzi huu unaanza tarehe 01 Oktoba, 2014.