Balozi wa Finland Azinduwa Kituo cha Msaada Wahanga wa Ukatili wa Kijinsia

Mkurugenzi wa Shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro(KWIECO) akimpokea Balozi wa Finland Tanzania Antila Sinikka aliyefika kwa ajili ya uzinduzi wa kituo cha msaada kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Watoa ushauri wa shirika linalotoa msaada wa kisheria na elimu ya haki za binadamu mkoani Kilimanjaro (KWIECO) wakiimba wakati wa ufunguzi wa kituo hicho. …