JK Ampa ‘Shavu’ Joseph Masikitiko TBS, Amwamisha Masilingi

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amemteua Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS). Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ambapo amemteuwa Lt. Gen. Charles L. Makakala kuwa Balozi …

Balozi Umoja wa Ulaya Atembelea Skimu ya Kiroka, Morogoro

Msimamizi wa mradi wa FAO kijiji cha Kiroka mkoani Morogoro, Ajuaye Sigalla, akitoa muhtasari wa maendeleo ya mradi FAO unaotekelezwa na wanakikundi wa Umoja wa Wakulima Kiroka (UWAKI) mbele ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Filiberto Sebregondi walipofanya …

Edward Lowassa Azungumza na Balozi wa Uingereza

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose aliyefika ofisini kwake leo kwa mazungumzo. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje,Mh. Edward Lowassa akiagana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania,Mh. Dianna Melrose mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Vanessa Mdee Asaini Mkataba Kuwa Balozi Samsung

KAMPUNI ya kielektroniki ya Samsung kwa mara ya kwanza imehusisha kampuni hiyo na msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania. Leo hii, Kampuni namba moja duniani inayoongoza kwa technolojia ya hali ya juu, Samsung wanayo furaha kumtangaza balozi wao mpya mwanamziki nyota, na mtangazaji wa Televisheni na radio Vanessa Mdee. Katika mkutano na wanahabari ulilofanyika hoteli, ya Hyatt Regency, iliyoko mjini …